WANYAMA WAWILI WA UFUNUO SURA YA 13
SEHEMU YA KWANZA: Mnyama akitoka katika bahari (ufunuo 13:1-10).
UTANGULIZI
Japo wengi husema kuwa kitabu cha ufunuo nikitabu kisicho eleweka (kimefubwa), lakini malaika anamwabia yohana katika maono (mnamo kati ya mwaka wa 95-105)
akisema; Akaniambia, Usiyatie muhuri(kuya fumba/kuya funga) maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. Ufunuo 22:10, hivyo kitabu cha ufunuo kinaeleweka kwa watu walio tayali kunyenyekea kujifunza kwa Mungu.
MADA KUUU:MYAMA AKITOKA KATIKA BAHARI.
Mungu ktk unabii unena kwa mifano Hosea 12 :10
Mnyama nimfano wa ufalme au Serikali yenye mamlaka ya juu kuliko falme nyingine Danieli 7:17,23
Anatoka baharini ufunuo 13:1,
Bahari au majimengi nimfano wa jamaa na makutano na mataifa na lugha mbali mbali, ufunuo 17:15
Ana vichwa saba na pembe 10 ufunuo 13:1
Pembe na vichwa ni mfano wa falme au serikali ndogo ndogo chini ya mamlaka iliyo kuu (ya kidunia) yaani mnyama.
Joka alimpa mamlaka ufunuo 13:2
Joka ni mfano wa ibilisi au shetani ufunuo 12:9 kwahiyo ufalme huo (mnyama) una pokea mamlaka kutoka kwa shetani.
Ni mfumo wa utawala ulio enea ulimwenguni kote ufunuo 13:3
Katika mwaka wa 538 AD Mfalme Justiniani wa Rumi(roma) alitoa amri ya kuwa Askofu wa Roma awe ndiye mkuu wa maaskofu, akajulikana kama Kaka mkubwa, alianza kujiinua taratibu hatimaye akasema lazima wamwite Baba (Papa kwa kiitaliano) nahatimaye Baba mtakatifu kama ilivyo ktk ulimwengu mzima wa hivi leo.
Inaonekana kuna maneno ya makufuru kutoka kwa huyu mnyama ufunuo 13:5
Luka 5:21 Yesu aliambiwa na wayahudi kuwa ana kufuru kwa sababu ya kusamehe dhambi(Wayahudi hawa kuamini kuwa Yesu ni Mungu), UPapa una dai kuwa na mamlaka ya kusamehe dhambi.Pia wana dai Papa hawezi kukosa. Soma katika PAPA NI NANI,Pd John Medri na Pd Magnus Lunyungu uk 30. Lakini biblia in sema tukisema hatuna dhambi twaji danganya wenyewe 1Yohana 1:8
Pia papa ana dai ku mwakilisha Yesu Duniani. Soma katika PAPA NI NANI,Pd John Medri na Pd Magnus Lunyungu uk 27 .kwakweli biblia inasema mwakirishi wa Yesu ni roho mtakatifu Yohana 16:7, 14:26,15:26
Mamlaka yake ilidumu kwa miezi 42 ufunuo 13:5;
Tafsiri ya Biblia inayoeleza siku moja = mwaka mmoja (Eze. 4:6, Hes. 14:34) ni dhahiri ya kwamba maneno haya yanamaanisha miaka 1260. Nyakati za zamani walihesabu mwaka mmoja kuwa siku 360. Mwezi mmoja unazo siku thelathini (Mwanzo 7:11,24, Mwanzo 8:4), miezi 42 x siku 30 = siku 1260, au miaka halisi 1260 katika historia. Tukianza kuhesabu miaka 1260 kwanzia 538, tunafika mwaka wa 1798 AD. Katika mwaka huu, Papa Pius wa sita alichukuliwa mateka na mfaransa Jenerali Berthier baada ya vita vikuu vya Ufaransa. PAPA NI NANI,Pd John Medri na Pd Magnus Lunyungu uk 97Ukatimia unabii wa: “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka” Ufunuo 13:10.
Somo hili tutaendelea na sehemu ya pili yake Mungu akijaria . Bofya kwenye neno "chapisha maoni" ili kuacha maoni yako kuhusu somo hili
JibuFuta